Tuesday, April 18, 2017

Mwigizaji wa filamu za James Bond Clifton James afariki dunia


Clifton James 1920-2017
Haki miliki ya picha Rex Features Image caption Clifton James, who has died aged 96, played Sheriff JW Pepper in two Bond films

Mwigizaji Clifton James, aliyeigiza kama Liwali JW Pepper kwenye filamu mbili za James Bond, amefariki dunia akiwa na miaka 96.

Alifariki karibu na mji wake aliokulia wa Gladstone, Oregon, siku ya Jumamosi kutokana na matatizo ya ugonjwa wa kisukari.

James alifahamika sana kutokana na uigizaji wake pamoja na Sir Roger Moore katika filamu za Bonds za Live and Let Die na The Man with the Golden Gun miaka ya sabini.

Binti yake Lynn amesema: ""Alikuwa mtu mpenda watu na mwenye uwazi sana. Alipendwa sana na kila mtu.""

Aliongeza: "Sidhani alikuwa na adui hata mmoja. Kwa kweli tulibarikiwa kuwa na yeye maishani."

Mwaka 1973, James aliigiza kama liwali wa Louisiana JW Pepper kwenye filamu ya Live and Let Die, ambao alifanikiwa sana kuigiza tukio la kukimbizana kwa boti.

His character proved so popular he was asked to reprise the role in 1974"s The Man with the Golden Gun, involving another car chase, in Thailand, and a scene where he gets pushed into water by a baby elephant.

Haki miliki ya picha Getty Images Image caption James aliigiza na Sir Roger Moore katika The Man with the Golden Gun

Uigizaji wake ulifurahisha mashabiki sana kiasi kwamba aliombwa kurejea tena mwaka 1974 kuigiza tena filamu ya The Man with the Golden Gun, tukio la kukimbizana kwa magari Thailand. Kwenye kisa hicho, alirushwa kwenye maji na mwanandovu.

Sir Roger ameandika: "Nasikitika sana kusikia Clifton James ametuachas. Kama JW Pepper aliboresha sana na kuongeza ucheshi katika filamu zangu mbili za kwanza za Bond."

James pia aliigiza katika msururu wa filamu za runinga wa Dallas, filamu za Superman II na The Bonfire of the Vanities.

Aliigiza mara ya mwisho mwaka 2006 katika filamu ya ucheshi ya Raising Flagg.

Alitarajiwa kuigiza katika filamu iliyopwa jina Old Soldiers, kwa mujibu wa IMDB.

Source: http://www.bbc.com/swahili/habari-39622901

No comments:

Post a Comment